6th ANNIVERSARY 8020 FASHIONS BLOGYESS!! LEO BLOG YENU YA 8020 FASHIONS IMETIMIZA MWAKA WAKE WA 6 TANGU IANZISHWE, NAOMBA NITOE SHUKRAN KWA MWENYEZI MUNGU, FAMILIA YANGU NA NYIE WASHABIKI WANGU PAMOJA NA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KWANI BILA NYIE 8020 FASHIONS SI KITU.

NINAFURAHA KUUBWA KUFIKA MIAKA HII SITA (6) KWANI SI KAZI NYEPESI PAMOJA NA CHANGAMOTO NYIIIIINGI, LAKINI PIA NINA MAFANIKIO MENGI SANA NIMEYAPATA KUPITIA HII BLOG, PAMOJA NA KUNIPA AJIRA MIMI SAMBAMBA NA VIJANA WENGINE TUNAOSAIDIANA KUENDELEZA LIBENEKE HILI BILA KUSAHAU BLOGGERS WENZANGU

NILIKUWA NA NINA NDOTO YAKUIKUZA  8020FASHIONSBLOG  KUENDANA NA TEKNOLOJIA MPYA ZINAZOBADILIKA KILA LEO DUNIANI, MBALI NA KUPOST PICHA TU NATAMANI SAANA KUITANUA ZAIDI,KUIBORESHA ZAIDI SAMBAMBA NA KUIFANYA 8020FASHIONSBLOG IPATIKANE KILA SEHEMU NA KWA KILA MTU 
NA SASA 8020 FASHIONS BLOG
INAPATIKANA KIGANJANI MWAKO KOKOTE ULIKO KATIKA UBORA ULEULE
WA KOMPUTANI

PIA UNAWEZA KUSCAN HII BARCODE KUPITIA SIMU YAKO NA UKAIPATA 8020FASHIONS BLOG


MWAKA JANA NILIFANYA SHEREHE TULIPOTIMIZA MIAKA MITANO NA NILISHUKURU SAANA KWA SUPPORT MLONIPA NYINYI WADAU SAMBAMBA NAMAKAMPUNI YALIYOJITOKEZA KUSHIRIKIANA NAMI KATIKA KUTIMIZA NDOTO YANGU
NA KATIKA NDOTO ZANGU NILIZOKUWA NAOTA NILIKUWA NAWISH TUWE NA PRODUCT ZA KIAFRIKA MBALI NA KUVAA TU VITENGE NA KANGA PIA TUJIREMBE NAVYO AMBAPO BACK 2 AFRIKA 
 'B2A' BRAND ZIKO TAYARI NA SOON ZITAINGIA SOKONI


NDOTO NYINGINE NILIKUWA NAOTA NI YAKUWAKUTANISHA WANAWAKE PAMOJA WA KARIBA TOFAUTI TUTAKAO  KAA NA KUZUNGUMZA MAMBO YETU ,TULE  TUNYWE NA TUCHEZA PAMOJA SAMBAMBA NA KUBADILISHANA MAWAZO, NA KUSHARE UJUZI NA KNOWLEDGE MBALIMBALI TULIZONAZO SI WAJUA NILICHO NACHO MIMI WEWE HUNA NA ULONACHO MIMI SINA.
HIVYO BASI NIKAONA HATUNA BUDI YA KUKUTANA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI IWE SIKU YETU MAHUSUSI KUSHEHEKEA PAMOJA, KUSHAURIANA MAMBO MBALIMBALI YENYE MANUFAA KWA JAMII YETU ; MAANA UKIMUWEZESHA MWANAMKE BASI UMEIWEZESHA JAMII NZIMA. 
WOMEN CELEBRATION IKAZALIWA


NA NAKUKUMBUSHA MAKAMPUNI,WAJASIRIAKALI AU WEWE  UNAYEPENDA KUSHIRIKIANA  KUWAKUTANISHA NA KUWAWEZESHA WANAWAKE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI AMBAPO TUTASHEREHEKEA TAREHE 3 MARCH MWAKANI TUWASILIANE
Call ::+255 784 418941  Email :: shamyomy@yahoo.com


HAPPY 6TH ANNIVERSARY
HERI YA X-MASS NA MWAKA MPYA
SHAMI MWASHA,'ZEZE' MAMA IQ
XOXO
Post Title : 6th ANNIVERSARY 8020 FASHIONS BLOG

6th ANNIVERSARY 8020 FASHIONS BLOG,

6th ANNIVERSARY 8020 FASHIONS BLOG

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...