WAANDISHI WA HABARI WA DRC WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.

Dar es Salaam 13 Des. 2012 ... Waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wamevutiwa na mafanikio yaliyopatikana kutokana na huduma ya M-Pesa nchini na kushangazwa na namna huduma hiyo ilivyofanikiwa kubadili maisha ya Watanzania.
Timu hiyo ya wanahabari ambao wapo nchini kwa ziara ya kujifunza namna huduma ya M-pesa inavyofanya kazi wamesema huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu ina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko makubwa kwa nchi za Afrika ukilinganisha na hali halisi ya uduni wa miundombinu barani humo.
Waandishi hao wako katika ziara ya siku nne nchini wameyasema hayo wakati wa ziara yao walioifanya katika makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania, na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kupokea maelezo ya namna huduma ya M-Pesa inavyofanya kazi.
Kampuni ya Vodacom DRC imeanza kutoa huduma ya M pesa hivi karibuni ikiwa na mwezi mmoja mpaka sasa. 
Mhariri Mkuu wa The Guardian on Sunday, Richard Mgamba(kushoto)akiongea na waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakati walipotembelea ofisi za The Guardian Limited,kwa kujifunza kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari,wapili kushoto ni Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambae alikuwa mwenyeji wa wageni hao

  Meneja wa vipindi wa Clouds TV Wasiwasi Mwabulambo(kushoto)akiwaonesha namna wanavyoandaa  vipindi baadhi ya waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakati walipotembelea ofisi za Clouds Media Group,mahususi kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari. 



 Mmoja wa watangazaji wa Clouds TV Ben Kinyaiya akipozi katika picha na Mwandishi wa gazeti la Antenne A la DRC Mamy Tambu.
 Mhariri Mkuu wa Clouds Joyce Shebbe, akiongea na waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),kuhusu namna wanavyofaidika na huduma ya M pesa wakati walipotembelea Ofisi za Clouds Media Group kwa ajili ya kujifunza namna ya kuweza kuelimisha jamii jinsi ya kutumia huduma ya M pesa kupitia vyombo vya habari.
Meneja wa vipindi wa Clouds Radio Sebastian Maganga,akiwafafanulia jambo waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),kuhusu namna wanavyofaidika na huduma ya M pesa wakati walipotembelea Ofisi za Clouds Media Group kwa ajili ya kujifunza namna ya kuweza kuelimisha jamii jinsi ya kutumia huduma ya M pesa kupitia vyombo vya habari.

 Meneja Mahusiano wa Vodacom DRC Fanny Kazadi,akifanyiwa mahojiano.
 Mwandishi Mwandamizi wa kituo cha Televisheni cha Channel ten,Bw.Dachi Mbwana akiongea na waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakati walipotembelea ofisi za Africa Media Group,kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari,wapili kushoto ni Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambae alikuwa mwenyeji wa wageni hao
 .Waandishi wa habari kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC),wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao wakati walipotembelea kituo cha Televisheni cha Channel ten na Magic FM, kwa ajili ya kujifunza namna ya kuelimisha jamii kuhusu huduma ya M-pesa inavyofanya kazi hapa nchini kupitia vyombo vya habari.
Post Title : WAANDISHI WA HABARI WA DRC WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.

WAANDISHI WA HABARI WA DRC WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.,

WAANDISHI WA HABARI WA DRC WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...