Wanahabari wajitokeza kwa wingi kununua mahitaji ndani ya maduka ya Shopaz Plaza kupitia M-pesa.



 .Meneja Uhusiano wa kampuni ya Vodacom-Tanzania, Matina Nkurlu (Kulia), akichagua bidhaa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari ndani ya duka la Shopaz Plaza Dar es Salaam. Waandishi wa habari walifika kwenye duka hilo , kufanya manunuzi ya bidhaa kwa kutumia  huduma ya M-Pesa. 
 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu , akiwaelekeza waandishi wa habari ndani ya duka la Shopaz Plaza namna huduma ya M-Pesa inavyotumika kwa manunuzi ya bidhaa ndani ya duka hilo. Waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini walifika dukani hapo kupata mahitaji mbalimbali na kulipa kwa kutumia huduma ya M-pesa.



Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Fidelis Felix, akilipia bidhaa kadhaa alizozinunua ndani ya duka la Shopaz Plaza  Msasani kwa njia ya huduma ya M-Pesa. Kampuni ya vodacom kwa kuanzia imeanza kutoa huduma ya kununua bidhaa kwa kutumia M-Pesa kwenye maduka ya Shoppers ya Msasani na Masaki, yote ya jijini Dar es Salaam


Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa mara ya kwanza wamejitokeza kwa wingi kupata mahitaji mbalimbali ndani ya maduka ya Shopaz Plaza jijini Dar es Salaam kwa kutumia huduma ya Mpesa.
Kampuni ya Vodacom Tanzania hivi karibuni,ilizindua rasmi matumizi ya huduma ya M-Pesa kwenye maduka ya Shopaz yaliyopo Msasani na Masaki,  ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuboresha huduma zake.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu, alisema programu hiyo imelenga kuwahamasisha waandishi wa habari kuweza kuelewa vizuri matumizi sahihi ya huduma hiyo kabla ya kuhabarisha wateja wengine.
"Lengo hasa ni kuwawezesha wateja kurahisisha manunuzi ya bidhaa zao mbalimbali, kwa namna hiyo hutakuwa na sababu ya kubeba  fedha taslimu, ni rahisi na salama kutumia, nawasihi na wateja wengine kujitokeza kutumia huduma hii," alisema Nkurlu Aliongeza kuwa azma ya Vodacom ni kuendelea kupanua wigo kati yake na wateja wake, katika muktadha wa ushirikiano katika kuwawezesha kupata huduma zake kwa urahisi zaidi.

Mmoja wa waandishi wa habari, ambaye pia ni mwandishi wa habari Mwandamizi wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Jerome Risasi, alisema amefurahia huduma hiyo kwa sababu ni rahisi na salama kuliko njia nyinginezo.
"Haya masuala ya kubeba fedha taslimu sasa yamepitwa na wakati, maana kama utabeba lundo la fedha mfukoni inakuwa ni kichocheo cha wezi na vibaka, nawashauri watanzania tubadilike na tuanze kutumia huduma hii ya  M-pesa kwa manunuzi ya bidhaa," alisema Risasi.

Huduma hiyo ni miongoni mwa huduma mbalimbali za malipo zaidi ya 200 zinazotolewa na Kampuni ya Vodacom nchini kwa kushirikiana na wabia wake mbalimbali.
Post Title : Wanahabari wajitokeza kwa wingi kununua mahitaji ndani ya maduka ya Shopaz Plaza kupitia M-pesa.

Wanahabari wajitokeza kwa wingi kununua mahitaji ndani ya maduka ya Shopaz Plaza kupitia M-pesa.,

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...