Wateja wa M pesa watakaonunua bidhaa Duka la Shoppers kupata muda wa maongezi bure.

Sasa M-Pesa imewarahisishia wateja wanaofanya manunuzi katika duka la Shoppers Plaza(Supermarket)ya Msasani na Masaki jijini Dar es Salaam. Vilevile utapata Tsh 1000 kama muda wa maongezi buremara baada ya kufanya manunuzi kupitia huduma ya M pesa.
 
Ili kuweza kulipia manunuzi dukani haponi rahisi sana, unachotakiwa kufanya:
 
Kwanza chagua bidhaa unayotaka kununua,na Muuzaji katika  kaunta ya malipo atakutaarifu jumla ya bei unayotakiwa kulipia. Hatua inayofuata ni kubonyeza *150*00# kwenye simu yako ili uweze kupata Menu ya M-Pesa halafu fuata hatua zifuatazo;
 
Bonyeza 5  kuchagua Nunua Bidhaa
 
·         Bonyeza 1 kama unafanya manunuzi  Shoppers ya Msasani au bonyeza  2 kama ni Shoppers ya  Masaki
·         Ingiza namba ya tili ambayo ni aidha 660660 kama ni  Shoppers Msasani au ingiza 607060 kama ni  Shoppers Masaki
·         Weka kiasi
·         Weka namba ya siri
·         Bonyeza 1 kuthibitisha au 2 kubatilisha
 
Baada ya manunuzi kufanyika, utapata  ujumbe mfupi au  SMS kukujulisha malipo yameshafanyika. Muuzaji atapata ujumbe wa manunuzi kwenye komputa yake na atakupatia risiti kama kithibitisho cha manunuzi.
 
 

Post Title : Wateja wa M pesa watakaonunua bidhaa Duka la Shoppers kupata muda wa maongezi bure.

Wateja wa M pesa watakaonunua bidhaa Duka la Shoppers kupata muda wa maongezi bure.,

Wateja wa M pesa watakaonunua bidhaa Duka la Shoppers kupata muda wa maongezi bure.

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...