KUWATUMIA WATAALAMU WA KITANZANIA WALIOKO UGHAIBUNI (DIASPORA) NA NDANI YA NCHI KUJENGA UWEZO NA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MUHIMU ZA SERIKALI
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano waTanzania
inakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko
ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa
Taifa.
Jamhuri ya Muungano wa
inakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko
ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye umuhimu kwa
Taifa.
Hapo awali,
Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo kwa sasa lengo
ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika pale tu ambapo wataalamu
wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.

Katika
kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa Kitanzania kwenye
maeneo yafuatayo:-

(i)
Mfumo
mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia na mafuta.

(ii)
Kuimarisha
matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika
kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.

(iii)
Kuboresha
utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa
kuhakikisha tunapata matokeo makubwa na
ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.

Wataalamu
watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo haya,
watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza kuongezwa iwapo
utendaji utaridhisha.

Mwito
unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni au ndani ya
nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na maelezo ya kwa nini
wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta.
Tumia anuani ifuatayo:-

Katibu Mkuu Kiongozi
Ofisi ya Rais, Ikulu
S.L.P. 9120
DAR
ES SALAAM.
ES SALAAM.
E.mail:chief@ikulu.go.tz
Post Title :
KUWATUMIA WATAALAMU WA KITANZANIA WALIOKO UGHAIBUNI (DIASPORA) NA NDANI YA NCHI KUJENGA UWEZO NA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI MUHIMU ZA SERIKALI
0 comments
Post a Comment