Vodacom yatembelea na kusaidia Sober House Pemba
Meneja wa kituo cha kutibu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) cha Chakechake Kisiwani Pemba Mohammed Kassim akisoma maelezo ya matumizi ya dawa ya kusafisha choo mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto)kwa niaba ya Vodacaom Foundation katika hafla iliyofanyika kituoni hapo mwishoni mwa wiki. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa pili kushoto). Vodacom Foundation imevipatia vituo vinne vya aina hiyo vya Wete na Chakechake vyakula na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya program ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Mratibu wa vituo vya kutibu watumiaji wa dawa za kulevya kuacha kutumia dawa hizo (Sober House) vya Wete Pemba Abdulwaheed Said akishukuru kwa msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kutoka Vodacom Foundation vilivtolewa kwa Sober House nne za Kisiwani Pemba. Kutoka Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa,Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon. Meneja wa Sober Hosue ya Chakechake Mohammed Kassim na Meneja wa Mahusiano ya Nje Salum Mwalim.Mkabidhiano hayo yamefanyika kwmishoni mwa wiki Mjini Chakecahke
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi dumu la dawa ya kusafishia choo kwa Meneja wa kituo cha kutibu kuachana na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) cha Mjini Chake Chake Kisiwani Pemba Mohammed Kassim. Wanaoshuhudia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kulia) na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon(wa pili kushoto). Vodacom Foundation imevipatia vituo vinne vya Wete na Chakechake vyakula na vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya program yake ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji.
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akikabidhi kiloba cha mchele kwa Meneja wa kituo cha kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo (Sober House) cha Chakechake Pemba Abdulwaheed Said kwa niaba ya Vodacom Foundation. Wanaoshuhudia ni Menejja wa Vodacom Foundation Grace Lyon Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(wa kwanza kushoto).Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kituoni hapo.
Post Title :
Vodacom yatembelea na kusaidia Sober House Pemba
0 comments
Post a Comment