Vodacom na Nokia yaja na ofa ya funga mwaka

*    Vodacom na Nokia yaja na ofa ya funga mwaka
*    Maelfu ya zawadi kushindaniwa kwa wanunuzi wa simu za Nokia
*    Pia kufaidika na SMS, muda wa maongezi na internet za  bure 
 

Dar es Salaam, Disemba 4, 2012 ... Wakati shamrashamra za maandalizi ya msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka yakiwa yanaendelea, Kampuni ya  Vodacom Tanzania na Nokia zimetambulisha ofa kabambe kukamlisha furaha ya kuelekea kufunga mwaka wa 2012.
Kampuni hizo kwa pamoja zimezindua rasmi shindano litakalomuwezesha mteja yeyote atakayenunua simu ya mkononi aina ya  Nokia, kujishindia zawadi mbalimbali papo kwa hapo, pamoja na kupata fursa ya kuingia kwenye droo kuu.Mteja atakayenunua simu ya Nokia na kisha kuweka muda wa maongezi wa aidha Tsh 1,000 au Tsh 1,500  atapata kifurushi cha BURE chenye muda wa maongezi  wa dakika 10, SMS 50  na internet ya MB10 kila siku kwa muda wa wiki moja. Kila simu ya Nokia itakayonunuliwa itakua na namba maalumu/kuponi ambayo mteja atatakiwa kutuma namba hiyo kwa SMS kwenda 15544 ili kuingizwa kwenye droo. Kila SMS itakayotumwa kwenda kwenye namba 15544 itatozwa gharama ya kawaida ya SMS.

Washimdi wa droo hizo zitakazokuwa zikichezeshwa kila siku watakuwa wakijishindia zawadi za simu, chargers, t-shirts na headphones zitakazotolewa kwa wateja kama zawadi za papo hapo.

"Ushiriki wa kubahatika kujishindia zawadi za papo hapo humuwezesha mteja kuingia moja kwa moja katika Droo kubwa ya mwisho itakayofanyika Januari 11, 2013 ambapo washindi watapata simu za kisasa za Nokia Lumia."Alisema Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa

Washindi wa zawadi za kila siku watachukua zawadi zao katika maduka ya Vodacom yaliyochaguliwa, ambapo watapatiwa huduma stahiki

Shindano hilo litafikia tamati ifikapo Januari 10, 2013, majira ya usiku, na Januari 11, 2012 ndiyo siku ambayo Vodacom na Nokia zitachezesha droo itakayoshirikisha washiriki wote wa shindano hili toka mwanzo, na kati yao mshindi atatangazwa.
Post Title : Vodacom na Nokia yaja na ofa ya funga mwaka

Vodacom na Nokia yaja na ofa ya funga mwaka ,

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...