VODACOM YAENDELEA KUWASAIDIA WALIOADHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI



Meneja wa Vodacom Zanzibar Mohammed Mansour akimkabidhi Katibu wa Taasisi ya Zanzibar Free Drug Badru Nassir Ali sehemu ya msaada wa vyakula na bidhaa nyengine za nyumbani kutoka Vodacom Foundation kusaidia nyumba kumi na moja za kusaidia waathirika wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo Kisiwani Unguja.Wanaoshuhudia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim(Katikati) na Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon. Hafla hiyo ilifanyika Mjini Zanzibar hivi karibuni. Msaada huo ni sehemu ya program ya Pamoja an Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji msimu wa Sikukuu za mwishoni mwa mwaka.






Meneja wa Vodacom Foundation Grace Lyon akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi msaada ya vyakula na bidhaa nyengine za matumizi ya nyumbani uliotolewa na Vodacom Foundation kwa vituo kumi na moja vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo. Kutoka kulia kwake ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim,xxxx, Meneja wa Vodacom Zanzibar Moh'd Mansour, Katibu Msaidizi wa Mtandao wa Free Drug Zanzibar Fatma Sukwa na Katibu wa Mtandao huo Badru Nassir Ali. Msaada huo ni sehemu ya Programu ya Pamoja na Vodacom ya kusaidia watu wenye mahitaji msimu wa Sikukuu za mwishoni mwa mwaka.



Baadhi ya watumiaji wa dawa za kulevya waliopo kituoni hapo kwa ajili ya kuachana na matumizi ya dawa hizo


Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na waanzilishi wa vituo na watumiaji wa dawa za kulevya mara baada ya kutoa msaada ya vyakula na bidhaa nyengine za matumizi ya nyumbani uliotolewa na Vodacom Foundation kwa vituo kumi na moja vya kusaidia watumiaji wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Post Title : VODACOM YAENDELEA KUWASAIDIA WALIOADHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI

VODACOM YAENDELEA KUWASAIDIA WALIOADHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI,

VODACOM YAENDELEA KUWASAIDIA WALIOADHIRIKA NA MADAWA YA KULEVYA NCHINI

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...