MTOTO AMWEZESHA MAMA KUSHINDA”MAHELA”




 Katika hali isiyo ya kawaida moja kati ya washindi wa promosheni ya” MAHELA” inayochezeshwa  na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania amebainisha kuwa utundu wa mtoto wake kuchezea simu umemuwezesha kushinda Shilingi milioni moja kutoka katika promosheni hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa pesa hizo katika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo yaliyoko Mlimani City jijini Dar es Salaam,  Bi, Ruth John Mungule Mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam amesema kuwa anaamini asinge kuwa mtoto wake kutumia ujanja kushiriki mchezo huo asinge weza kushinda pesa hiyo.
“Siku ya jumatatu asbui wiki iliyopita mtoto wangu aliniomba kutuma message ili kushiriki hii Vodacom MAHELA, nilimruhusu siku iliyofuata juma nne nilipigiwa simu kutoka Vodacom kuambiwa kuwa nimeshinda shilingi Milioni moja, haikuwa rahisi kuamini lakini hadi leo nimefika hapa na kukabidhiwa fedha zangu nimeamini ni kweli.




Mshindi mwingine alieshinda katika droo iliyo chezeshwa jana (jumatatu) ambaye ni askari polisi, Bi Liberata Karigita Mkazi wa Kilwa Road Balax, jijini Dar es Salaam, katika mahojiano yake kwa njia ya simu na Meneja wa mawasiliano wa Vodacom wakati wa kuwatafuta washindi wa droo ya pili alisema kuwa muda mwingi alipokuwa akiwasihi wenzake kushiriki walimcheka na kumbedha.
“Mara nyingi nilipokuwa nashiriki kwa kutuma message Askari wenzangu walinicheka na wengine kunibeza kuwa napoteza fedha zangu bure lakini leo Vodacom wamenitoa aibu na nimwshinda milioni tano nashukuru sana Vodacom, alibainisha Askari huyo.
“Tunawashukuru sana wateja wetu kwa kuitikia wito wetu na kushiriki vizuri katika promosheni yetu hii ya VODACOM MAHELA, Ninawasihi wateja wengine hata ambao hawajajiunga na Vodacomm kuhakikisha wanajiunga na kushiriki katika promosheni hii, MAHELA, ni kwa watanzania wote, alisema Rukia Mtingwa, Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.Hadi kufikia sasa tayari kampuni ya Vodacom kupitia promosheni yake ya Vodacom Mahela imepata jumla ya washindi 31 ambapo mshindi wa jumla atajishindia milioni 100 katika droo kubwa itakayo chezeshwa baada ya siku tisini za muda wa promosheni hiyo.
Post Title : MTOTO AMWEZESHA MAMA KUSHINDA”MAHELA”

MTOTO AMWEZESHA MAMA KUSHINDA”MAHELA”,

MTOTO AMWEZESHA MAMA KUSHINDA”MAHELA”

0 comments

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...